Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Ufafanuzi wa Klabu

 

Tuanze!

Amua kuhusu jina la klabu.


Mnaweza kuipa jina klabu yenu kwa namna yoyote mnayotaka, inabidi tu itii masharti rasmi ya majina na vizuizi.

Hakuna haja ya kuweka "Agora" kwenye jina la klabu yenu. Kwa mfano, klabu yenu inaweza tu kuwa "Wazungumzaji wa Kiwango cha Juu wa Paris".

Nembo ya Klabu

Kwasababu ya nyenzo nyingi sana (kama vile medali, vyeti, fomu za utathmini, nk.) zinatengenezwa, na pia kuzuia kuchanganyika kwa nyenzo ambazo klabu zimetengeneza na nyenzo rasmi za Taasisi, vilabu vyote vinahitajika kuwa na nembo yao maalum. Pia, kuwa na nembo ya klabu inasaidia kuongeza urafiki kati ya wanachama na inafurahisha zaidi mtakapokuwa mnashiriki matukio ya nje.

Kuna chaguo mbili:

  • Mnaweza mkatengeneza nembo yenu ya klabu maadam ifuate mwongozo wa chapa.
  • Tunaweza kuwatengenezea nembo otomatiki pale mtakapounda klabu, kutokana na mtindo wa sanifu ambao unajumuisha nembo ya mraba ya Agora na jina la klabu.
    Kwa mfano, kama klabu inaitwa "Amman Speakers", nembo ambazo tunatoa zitakuwa kama hizi (isipokuwa tunazitoa kwenye  that we provide them in very high resolution).

Logo 1

Logo 2

 

Unaweza ukaanza na nembo ambayo tumetengeneza otomatiki, alafu ukabadilisha pale klabu itapoanza kufanya shughuli zake.

Amua sifa bainifu za klabu yako.

Kinachofuata, unahitaji "kuipa sura" klabu kwa kuamua  baadhi ya sifa za msingi. Karibia zote zinaweza zikabadilishwa pale klabu itakapoanza kufanya shughuli zake, kwahiyo usizuiliwe na hatua hii.

 

Aina ya klabu

Agora ina aina za klabu tofauti, kila moja ina sifa bainifu tofauti, mahitaji, na ada. Aina inayotumiwa sana ni Klabu ya Umma, ambayo inakubali kila mtu kuwa mwanachama, na ndio ambayo tunapendekeza. Klabu za Umma zina uhuru kamiilifu kutengenezwa na kutokulipa ada ya aina yoyote kwa Agora Speakers International.
 

Mikutano ya Mitandaoni au Uso kwa Uso?

Klabu inaweza kukutana uso kwa uso, mitandaoni pekee, au mchanganyiko wa zote mbili.

Kwenye suala hili, tunapendekeza kuwa na klabu ya kawaida (ya uso kwa uso) ambayo mara nyingine inakutana mtandaoni. Mikutano ya mitandaoni inaruhusu wanachama kutoka duniani kote kushiriki na ni fursa nzuri sana ya kukutana na watu wapya, kupata maoni mapya ya nje, na inawaonyesha tamaduni tofauti, mawazo na lafudhi za lugha. Kuongezea, kuwa na mkutano mtandaoni inarahisisha kuandikisha wanachama wapya kwasababu inakuwa rahisi kwa watu wadadisi "wanaosita kufanya maamuzi" ya kutembelea klabu bila juhudi nyingi au wajibu.

Ujuzi kamili wa kielimu unapatikana kwenye klabu ambayo wanakutana uso kwa uso tu, kwahiyo tunapendekeza chaguo hili. Pia, kumbuka kuwa baadhi ya miradi ya kielimu inaweza isifanywe kwenye mtandao au kuwa na mahitaji ya nyongeza kwenye suala hilo.

Ni wazi kwamba, klabu vya uso kwa uso vinaweza kubadilika na kukutana mitandaoni kwenye hali za kipekee kama janga la 2020.

Ni changamoto kusukuma gari na kulifanya lisogee. Lakini, pale litakapoanza kusogea, ni rahisi kuliacha katika hali hiyo.

Klabu ni sawa na hii na pia ina uzito mwingi - inachukuwa juhudi kupata klabu imara na ambayo inakutana mara kwa mara. Kama una klabu ambayo inakutana uso kwa uso na mara kwa mara, na hali ya kipekee ikajitokeza, ni bora zaidi kubadilika kwenda mikutano ya mtandaoni na kuendelea hivyo kuliko kusimama mikutano yote kwa ujumla na alafu mjaribu kukutana tena.

 

Mahali rasmi pa klabu.

Hata kama klabu ni ya mtandaoni tu, lazima iandikishwe kwa ajili ya shughuli za shirika kwamba ipo au inapatikana kwenye mji au eneo maalum - moja ambalo wanachama wengi waanzilishi wanaishi.

Kumbuka kuwa hii ni moja ya vitu vichache ambavyo haviwezi kubadilishwa pale klabu itakapoandikishwa. Klabu ambayo iliandikishwa ipo Paris, Ufaransa, haiwezi kubadilishwa baadae kuwa ipo Rio de Janeiro, Brazili.

 

Ratiba ya Mkutano

Ni siku gani kwenye wiki mtakuwa mnakutana? Klabu za Agora Speakers lazima vikutane japo mara moja kwa mwezi, isipokuwa kwenye likizo ya kiangazi. Bila shaka, mnaweza mkakutana mara nyingi zaidi - mara moja ndani ya wiki mbili, au hata kwa wiki. Baadhi ya klabu zinakutana mara nyingi zaidi - mara mbili kwa wiki!. Vyovyote vile, ni vyema zaidi kama klabu yenu itakuwa na ratiba nzuri ya kukutana.

Japokuwa kwa kawaida, klabu zinachagua ratiba ya kukutana ambayo ni mara mbili kwa mwezi (kama vile "kila Jumatano ya kwanza na ya tatu"), kama klabu yako ni ya Umma, tunapendekeza mkutano kila wiki. Hii itafanya vitu kuwa vigumu zaidi mwanzoni kwasababu ni vigumu kwa watu kuwa na aina hiyo ya wajibu. Kama unaanza na wanachama waanzilishi 20 au 30, kutakuwa na mikutano ambayo utakuwa na wanachama 4 au 5 tu ambao wanahudhuria. Hiyo ni sawa - kama kiongozi wa klabu, utahitaji pia kukabiliana na masuala ya aina hii.

Lakini, baada ya muda, klabu ambayo inakutana kila wiki itakua haraka kwasababu ratiba ipo dhahiri zaidi kwa wanachama watarajiwa. Kama klabu inakutana kila Jumatano, basi kila mtu anajua kuwa kama ni Jumatano, kutakuwa na mkutano. Lakini, kama klabu inakutana kila "Jumatano ya kwanza na ya tatu", itamlazimu mtu kuangalia kalenda Jumatano ipo ndio mkutano unaofuata utakuwa, alafu itakuwaje kama kuna Jumatano ya tano kwenye mwezi, alafu inakuwaje kama Jumatano ya kwanza ilikuwa ni likizo na je mkutano umepotea au umesogezwa kwenda Jumatano ya pili, nk.

Mkiamua kuwa klabu itakutana kila wiki, ni wazo zuri kuwakumbusha wageni kuwa haina tatizo kama wasiopohudhuria kila wiki.

 

Mahali pa Mkutano

Kama klabu itakutana uso kwa uso, utahitaji mahali pa mkutano ambapo panafaa. Tutazungumza kuhusu mahali pa mkutano baadae kidogo.


Lugha zitakazotumika ndani ya klabu.

Kama ilivyoelezwa kabla, tunahimiza vilabu vya Agora Speakers kutumia sio tu Kiingereza lakini pia lugha za kiambo. Unaweza ukawa na klabu ambayo inatumia tu lugha moja au klabu ambayo inabadilisha lugha kwenye mikutano, au klabu ambayo inaruhusu uchaguzi wa lugha kutumiwa kwenye mkutano mmoja.

Wakati wa kuchagua lugha ya klabu, zingatia kama nyenzo za kielimu za Agora zinapatikana katika lugha hiyo. Tunaweza kuongeza lugha kwenye wiki, na kutafsiri ni mara nyingi kwa kujitolea, kwahiyo kama unataka klabu yako itumie lugha ambayo haipo kwenye wiki, tafadhali fikiria kusaidia kutafsiri nyenzo kwanza.

Isipokuwa kama unategemea wanachama wako wote wajue lugha zote zinazotumiwa, tunapendekeza kuwa kila klabu izingatie kutumie lugha moja tu (sio lazima iwe Kiingereza). Kama klabu inachanganya lugha mbili kwenye kipindi kimoja (tuseme Kihispania na Kiingereza), baadhi ya wanachama wanaweza wasielewe nusu ya maudhui na wakahisi kutengwa. Kwa kuongezea, inamchosha mzungumzaji pia kuona kwamba baadhi ya hadhira hawapo makina kwasababu hawaelewi lugha ambayo anatumia.

Kama klabu inabadilisha mikutano kati ya lugha mbili, basi kinachotokea ni kuwa wanachama wataenda kwenye kipindi ambacho lugha inayotumiwa wanaielewa vizuri zaidi - kitu ambacho kinatenganisha klabu.
 

 

Ada ya klabu itatozwa kwa wanachama.

Japokuwa Agora haitozi ada yoyote ile kwa klabu za wazi za umma, klabu yenu inaweza ikawatoza wanachama ili kusaidia kuiendesha kiufanisi. Tafadhali kumbuka kuwa kama utatoza ada, unahitaji kutii masharti ya fedha za klabu zote.

 

Washiriki wasio wanachama

Kuna aina tatu za watu wasio wanachama ambao wanaweza kutembelea klabu, na unahitaji kuamua ni majukumu gani ambayo utaruhusu wafanye kwenye mkutano.

Mwanachama asiye mwenyeji ni mwanachama wa klabu nyingine ya Agora Speakers. Unaweza kuamua utaruhusu "wageni" hawa maalum wachukue jukumu lolote lile isipokuwa hotuba zilizoandaliwa.

Tunawahimiza klabu kuruhusu mwanachama yoyote yule wa Agora kuruhusiwa kufanya jukumu lolote kwenye klabu nyingine yoyote ya Agora. Hii inasaidia kujenga kujiamini,kwasababu wanachama wanajifunza uzungumzaji wa mbele ya hadhira mbele ya hadhira nyingi tofauti na sio tu wanachama wa klabu yao ya nyumbani.

Wageni, kwa upande mwingine, watu kutoka hadhira ya kawaida ambao sio wanachama wa klabu yoyote, na muda mwngi, hawajui klabu inahusu nini na wanataka kudadisi kuhusu shirika. Tunawahimiza kuwaruhusu kufanya majukumu rahisi kama vile wazo la siku au kushiriki kwenye mada za hapo kwa hapo ili wapate kujua kuhusu uzungumzaji wa mbele ya hadhira.

Wawakilishi wa Shirika. Wawakilishi wa Shirika ni wanachama wa bodi ya uongozi, na pia mabalozi wa Agora. Kwa kushiriki, inawalazimu wafuate masharti sawa kama wanachama ambao sio wenyeji. Kwa maneno mengine, vyeo pekee haviwapi haki ya kushiriki kwa kipekee.
 

Klabu za Umma zinatakiwa kukubali wageni na wanachama wasio wenyeji kwenye mikutano yao, kulingana na nafasi iliyopo kama mkutano ni wa uso kwa uso kwenye ukumbi.

Kwa kuongezea, klabu zote zinatakiwa kukubali kutembelewa na wawakilishi wa Shirika na mabalozi kupata mwongozo na kuhakikisha kuwa klabu zote zinafuata uendeshaji wa Agora.

 

Taarifa za mawasiliano za klabu


Klabu lazima zichapishe aina mbili tofauti za mawasiliano za klabu, moja yao lazima iwe barua pepe au namba ya simu. Hii taarifa itakuwa wazi kwa umma.

Hii ni baadhi ya mifano ya mchanganyiko inayofaa na isiyofaa

  • Barua pepe na Facebook
  • Namba ya simu na tovuti 
  • Namba ya simu na barua pepe
  • Tovuti na Facebook
  • Instagram na Facebook
  • Instagram na namba ya simu

Utahitaji pia kumpa jukumu hili mtu maalum ili awe mtu wa mawasiliano ya klabu. Mtu huyu wa mawasiliano anaweza akawa mwanachama yoyote (sio lazima awe ofisa wa klabu) ambaye atakuwa na kazi ya kujibu taarifa zinaulizwa na watu waliovutiwa.

Rekodi za Mikutano

Kitu kingine kimoja cha muhimu sana ambacho unahitaji kuamua ni kwamba je mikutano irekodiwe na ipigwe picha na kama wanachama ana haki ya kuomba kutokuwepo kwenye utaratibu huo.

Uamuzi wowote ule, hakikisha kuwa unaelezewa vizuri kwenye tovuti zote za klabu, nyenzo za matangazo, na posti za matukio.

Tunapendekeza kuwa mikutano yote irekodiwe na ipigwe picha na zitakapokuwa tayari ziwekwe wazi kwa umma. Hii inatoa mwendelezo wa maendeleo mazuri ya jinsi wanachama wanavyoendelea na inasaidia kuwavutia wanachama wapya kuja kujiunga kwenye klabu.

Kama klabu itaamua kufuata pendekezo la hapo juu, basi ni muhimu kuwa aidha Mwezeshaji wa Mkutano, au Kiongozi wa Mkutano, au Mpiga video, au Ofisa wa Klabu yoyote aseme wazi mwanzoni mwa mkutano (wa kila mkutano) -  kabla rekodi haijawashwa - kuwa mkutano wote utarekodiwa. Hii ni muhimu kwasababu mkutano unaweza ukawa na wageni ambao hawalijui hili suala (japokuwa, wageni wanatakiwa kupewa taarifa hii kabla ili kuepuka kupoteza muda wao kama hawataki). Agora Speakers inahitaji klabu zote zitii mfumo wa faragha wa GDPR wa Ulaya (haijalishi mahala au wapi ambapo klabu ipo), hii inamaanisha kuwa taarifa inatakiwa kuelezea:

  • Kuwa mkutano utarekodiwa
  • Dhumuni la kurekodi
  • Wapi taarifa zitapostiwa/zitawekwa
  • Kama kuwa uwezo wa kutokuwepo/kutokutokea (au hapana) na jinsi ya kufanya hivyo.

Kwa mfano, hii inaweza ikawa sampuli ya tamko:

"Habari zenu,  Kama kwenye mikutano yote, nahitaji kuwataadhari kuwa mkutano utapigwa na utarekodiwa. Tunafanya hivi ili wanachama wote waweze kuona maendeleo yao na pia kuonyesha klabu yetu kwa wengine. Video zitawekwa kwenye channeli ya klabu ya Youtube na vitakuwa wazi kwa mtandaoni kwa ujumla. Tutatuma pia baadhi ya video zetu bora na hotuba kwenda Agora Speakers International. Tafadhali jua kwamba pale zitakapowekwa, hatutaweza kufanya kitu chochote kusimamisha uenezi wa video.

Kwa bahati mbaya, kuhariri video ni kazi inayochukua muda mwingi sana, kwahiyo tunaomba kama kuna mtu ambaye hataki hotuba yake irekodiwe aseme dhahiri mwanzoni mwa hotuba ili tusimamishe kurekodi. Kama ukibadilisha maamuzi baadae, chaguo lako ni kuhariri video mwenyewe na vifaa vyako na kutupatia video ya mwisho ndani ya wiki moja baada ya mkutano.

Pia, tafadhali kumbuka kuwa hii inawahusu ambao wanachukua jukumu amilifu tu. Kama wewe ni sehemu ya hadhira, hatuwezi kukutoa kwenye video, kwahiyo chaguo lako ni moja tu, kama hautaki kuwepo kwenye video yetu, ni kuondoka kwenye mkutano sasa hivi. Mtu yoyote anayebaki anatoa idhini kuwa uwepo wake urekodiwe na usambazwe kwa umma
."

 

Hamna aibu ya kuwa na "sera ya kukataa kutokuwepo". Kwani, Agora na klabu wote wanatoa huduma yenye thamani kubwa kwa mtu yoyote anayetaka kujiunga, kwa gharama ndogo (au bure kabisa, kama klabu haitaki ada yoyote). Kozi za kitaalam kwa seti sawa za ujuzi zinaanza kuanzia dola elfu kadhaa.

 

Kanuni za kufatwa zinazotumiwa kwenye klabu

Ukiachana na mikutano ya kawaida ya kielimu, klabu yenu itatakiwa kuwa na mikutano ya kujadili masuala ya aina tofauti:

  • Matumizi ya fedha za klabu
  • Uchaguzi wa maofisa wa klabu
  • Taratibu za Nidhamu
  • Kubadilisha vipengele vyovyote vya klabu kutoka sehemu hii
  • ...mada zingine zozote za klabu

Japokuwa baadhi ya sehemu za jinsi vitu vitakavyoendeshwa wakati wa mikutano hii vipo kwenye Katiba ya Klabu ya Agora (kama vile jinsi kura zitakavyohesabiwa na jinsi waliowengi watakavyohesabiwa), klabu inahitaji kuamua seti za kanuni/masharti ambayo yatatumiwa kuhakikisha mikutano inenda sawa:

Hii hapa ni baadhi ya sehemu ambazo unaweza kuchagua kutoka:

Kama klabu yako inaamua kuchagua seti za kanuni tofauti na hizo ambazo zimependekezwa, tafadhali kumbuka kuwa seti za kanuni LAZIMA:

  • Inawapa wanachama wote wa klabu umuhimu ulio sawa
  • Inawapa wanachama wote wa klabu nafasi sawa ya kuwasilisha, kusapoti, kupinga, na kutoa mada au mawazo.
  • Inawapa wanachama wote fursa sawa na muda wa kushirika kwenye mikutano bila kuogopesha au woga wa kutokubaliana.

 

Aina ya Maudhui ya Hotuba

Jambo la mwisho ambalo utataka kuamua ni aina ya maudhui ya hotuba ambayo yanaruhusiwa kwenye klabu. Kuna masuala mengi ambayo unaweza ukataka kuweka dhahiri. Kwa mfano, unaweza ukataka kuwa na klabu ambalo ni maalum kwa ajili ya Historia ambapo hotuba za mada za kihistoria tu ndio zinakubaliwa. Mbadala, unaweza ukawa na klabu ambayo inajishughulisha na kujifunza kufanya mauzo tu. Kama unataka kuweka vizuizi vya aina ya maudhui ya hotuba ambayo yanaruhusiwa, hakiksha kuwa unasoma makala maalum kuhusu kanuni zinazoongoza hii.

 

Usajili wa Kisheria

Maamuzi ya mwisho ni kama unataka kuendelea na usajili wa klabu kisheria na msajili wa mashirika yasiyo ya faida. Mlolongo huu kwa kawaida ni mgumu, hautakiwi kuchukuliwa kirahisi na unaweza ukangusha utaribu wote wa kuunda klabu. Kwa bahati mbaya, hatuwezi kutoa taarifa maalum kuhusu kama inahitajika kwa klabu yako na jinsi inavyofanywa - utahitaji ushauri wa mtaalam kwenye eneo lako. Kwenye suala hili kwa kawaida, tuna mapendekezo haya matatu (yasichukuliwe kama ushauri wa kisheria):

  • Kama sheria inakubali, jaribu kuanzisha klabu na kuendesha na iwe imara kabla haujanza mlolongo wa kusajili kisheria. 
     
  • Tunachukulia klabu kama "makundi ya faragha ya kujisomea" - seti ya watu binafsi wanakutana baada ya muda fulani kusoma na kujifunza kwa pamoja baadhi ya maarifa, haina tofauti na jinsi wanafunzi ndani ya darasa wanavyokutana kusoma na kujiandaa kabla ya mtihani. Baadhi ya mikutano hii inakuwa na gharama (kama vile kukodi chumba cha kusomea) ambazo zinahitaji kuchangiwa. Tafiti kama eneo lako linahitaji kundi kama hili liwe limesajiliwa kisheria.
     
  • Klabu zinajitegemea zenyewe; hazihusishwi kisheria na Shirika la Agora Speakers International. Kwahiyo, usajili wowote unatakiwa ufanywe kama shirika huru la kiambo na sio "tawi", "muwakilishi", au "sehemu" ya shirika la kigeni.
     
Klabu za Umma, Klabu za Manufaa ya Umma, na Klabu zenye Vizuizi hazihitaji kujiandikisha kama mashirika yasiyo ya faida. Kama wanataka kufuatilia kujiandikisha kisheria, lazima iwe kama shirika lisilo la faida.

Tafadhali kumbuka kuwa muda mwingi, kujiandikisha kisheria inaamnisha kuwa utahitajika kununua bima ya madhara ya raia. Tena, hii ni moja ya maeneo ambayo hatuwezi kukupatia taarifa au kukusaidia kwa njia yoyote ile - mtafute mtaalam wa sheria katika eneo lako.

 

Umesahau uamuzi?


Tumia fomu hii muhimu kutoka Kitengeneza Rasilimali chetu kurekodi maamuzi yote yaliyofanywa na hakikisha kuwa haujasahau kitu chochote.

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:39 CEST by agora.